VIDEO: Jiandae Kuendesha Ndege Yako. Gari la Kwanza kwa Matumizi Binafsi. Halihitaji Njia ya Kuruka Ili Iweze Kupaa


Je ungependa tena kutosumbuliwa na foleni za mjini pindi itapofika mwaka 2015..? Ndio! hili ni gari ambalo unaweza kuliendesha barabarani huku pia likiwa na uwezo wa kupaa angani.

Gari hili halihitaji njia ndefu ya ndege kuweza kuruka na kutua kama ndege nyingine zinavyofanya.

Kampuni moja nchini Uingereza iitwayo Terrafugia ametambulisha aina mpya ya gari inayopaa (flying car), gari ambalo linaweza kuwa ndege binafsi yenye viti viwili, matairi manne na mabawa yanayofunga na kufunguka ili kuweza kuendeshwa kama gari la kawaida barabarani.

Gari hili imeelezwa kwamba linategemea kuingia sokoni kwa matumizi ya jamii kuanzia mwaka 2015.

Unazungumziaje uvumbuzi huu....?

Angalia Video hapo chini....!


No comments:

Post a Comment