Snoop Lion Abadili Tena Jina

Snoopzilla
Rapa na Muimbaji ambaye pia ni Muandishi wa nyimbo, jina lake halisi likiwa ni Calvin Cordozar Broadus, Jr. amebadili jina kwa mara nyingine tena!

Mara ya kwanza alikuja na jina la Snoop Doggy Dogg, halafu Snoop Dogg, Snoop Lion na sasa anajiita Snoopzilla.

Ikiwa hata mwaka haujaisha toka alivyojiita Snoop Lion, rapa huyo amesema amebadili jina ili aweze kwenda sawa na muelekeo mpya wa muziki anaoufanya sasa, mziki wenye mradi akiwa na Funk unaokwenda kwa jina la 7 Days of Funk, ambapo kwa pamoja na Dam-Funk wanategemea kutoka na album ya kwanza mnamo Desemba 10 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment