Mke wa Timbaland Afungua Kesi Kudai Taraka Baada ya Miaka Mitano ya Ndoa

Monique & Timbaland
Mke wa mtayarishaji wa muziki Timbaland, ambaye wapo kwenye ndoa kwa miaka mitano sasa aitwaye Monique Mosley, amefungua kesi ya kudai taraka baada ya miaka mitano ya ndoa.

Kwenye faili la madai ya taraka hiyo ambalo mtandao wa TMZ imelipata, Monique anahitaji msaada kwa ajili ya huduma za watoto wake, wa kwanza ni mtoto wao wa miaka mitano na pia kwa ajili ya mtoto wake wa kike mwenye miaka kumi ambaye alimpata kwenye mahusiano yake ya nyuma.

Timbaland ana utajiri unaokadiliwa kufika $80million kwa mujibu wa mtandao wa watu mashuhuri.

No comments:

Post a Comment