''Nililipwa $2500 USD Ili Nimuuwe 2Pac'' - Dexter Isaac | Habari Kamili

Marehemu 2Pac
Mtu mmoja ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha maisha pamoja na miaka mingine 30 ya mauwaji na uporaji, anayeitwa Dexter Isaac amesema yeye ndiye aliyehusika kumpiga risasi Tupac Shakur kwenye Quad Studios ndani ya Manhattan mnamo mwezi November 1994, huku akiongeza na kusemea kuwa pia alihusika kwa cheni ya iliyosababisha mauwaji ya wote wawili yaani Shakur na Notorious B.I.G., ambaye mwanzoni ndiye aliyetuhumiwa moja kwa moja na njama za kifo cha Tupac.

Kwenye taarifa yake jamaa huyo alisema alilipwa $2,500 na James “Jimmy Henchman” Rosemond, mdau mkubwa wa muziki ambaye kwa sasa ni CEO wa Czar Entertainment na ni meneja wa The Game.

Kwenye taarifa hiyo, Isaac ameomba msamaha kwa familia ya Tupac na Biggie na akasema aliamua kukaa kimya mpaka sasa sababu ukomo wa wa kesi hiyo kwa yeye kuhukumiwa umeshakwisha na kwamba hawezi kuhukumiwa kutokana na shambulio hilo.

Isaac pia ameelezea kujuta kwake kwa kujihusisha na Rosemond, ambaye anaamchukulia kama mtu “mbaya.”

Rosemond kwa sasa yupo mafichoni akiwa anatafutwa na DEA na federal marshals kwa kuhusishwa na usafirishwaji wa madawa ya kulevya.

No comments:

Post a Comment