BARUA: Mke wa Boyfriend Wangu ni Bosi Wangu Mpya, Nifanyeje...?


Wapendwa Wasomaji....

Nimechanganyikiwa, kwa maana hivi karibuni nimetoka kupata kazi na nimekuja kugundua kwamba bosi wangu ni mke wa boyfriend wangu.

Siku za nyuma tumekuwa tukikutana na mwanamke huyu, cha kushangaza ni hili nililokutana nalo, hakika limenipa mshtuko, mara baada ya kugundua kwamba mke wa boyfriend wangu ndiye bosi wangu mpya.

Ila kitu cha kushangaza juu ya hili ni kwamba, toka nimejiunga na kampuni hiyo, mwanamke huyu hajajionyesha kama ni mtu ambaye mimi na yeye tunafahamiana toka siku za nyuma.

Hakika naogopa, hivyo swali langu ni hili; Je napaswa kujifanya kwamba kila kitu kipo sawa na kwamba simfahamu huyu mwanamke..? Au bora nitimke zangu, niache kazi na kutafuta kazi sehemu nyingine...?

Kitu kinachonichanganya zaidi ni juu ya huyu mwanaume tunayechangia, kamwe sioni kama kuna uwezekano wa mimi na yeye kuachana. Na sehemu ninayofanyakazi kiukweli masirahi yake ni mazuri ambayo kila mtu angependa kufanya kazi hapo.

Tafadhali naomba ushauri, nini napaswa kufanya...?

No comments:

Post a Comment