PICHA/VIDEO: Kanye West Amleta Mtu Anayefanana na Yesu Kwenye Steji


Rapa, Kanye West ameanza ziara ya 'Yeezus' ndani ya Seattle mnamo siku ya Jumamosi October 19 na kabla hajaimba wimbo wake wa Jesus Walks, alitokea mtu aliyevaa kama Yesu kwenye steji.

Kanye akatania kwa kuuliza "Yesu mweupe, je ni wewe?… Oh, shit!". Kisha akavua kipande cha sanamu aliyokuwa ameivaa kichwani na kusema amekuwa akimtafuta Yesu kwa kipindi chote cha show hiyo.

Baadae, Kanye na wacheza show wake wa kike walimuinamia kwa mtu huyo anayefanana na Yesu ambaye alionekana kama amesimama kwenye kilele cha mlima.

Jamaa huyo akajibu kwa kusema kwamba alikuwa pale kwa muda wote, na Kanye akaanza kuimba wimbo wake wa mwaka 2004 uitwao Jesus Walks.

Kendrick Lamar alifungua show hiyo huku akiimba nyimbo nane zikiwemo zile za kwenye album yake ya "good kid, m.a.a.d. city".




Cheki tukio hilo kwenye Video hii...

No comments:

Post a Comment