Kundi la wavulana 17 wenye umri wa wastani wa miaka 10 walifungua macho ya watu mara baada ya asubuhi moja kuonekana maeneo ya shule yao wakiwa wamevaa sketi walizoazima.
Muandamanaji Tyrone Evelyn, 15, alisema kundi hilo toka shule ya Whitchurch ndani ya Cardiff nchini Uingereza, litaendelea na kampeni yake kwa ajili ya kudai mabadiliko.
Alisema: “Hii ni sahihi kwa hali ya hewa - hatutaki kusikia joto na kusumbuka.
“Kwa kipindi cha siku za hivi karibuni nimekuwa nikipata maumivu ya kichwa na ngozi kuwashwa sababu ya imekuwa ni joto sana.
“Waschana wanavaa sketi, kwa hiyo sioni kwanini na sisi tusivae sketi. Ni maandamano sahihi.”
Tyrone na rafiki zake walivaa suruali wakiwa wanakwenda shule huku sketi wakiwa wamezificha kwenye mabegi baada ya kushukiwa na baadhi ya walimu juu ya mpango wao wa kuandamana, mpango ambao waliuandaa kupitia Facebook.
Cheki picha zaidi hapo chini....
“Waschana wanavaa sketi,
kwa hiyo sioni kwanini na sisi tusivae sketi.
Ni maandamano sahihi.”
Muandamanaji
Tyrone
Japo neno moja kwa hawa watoto...
No comments:
Post a Comment