Man United Wanapoteza Muda Wao kwa Fabregas - Gerard Pique

Cesc na Pique
Barcelona FC wameendelea kubaki na msimamo wao wa kutotaka kumuuza kiungo wao wa Kispanish Cesc Fabregas, huku klabu ya Manchester United wakiwa kwenye msimamo wa kumtaka kwa kila hali.

Mnamo siku ya Jumatatu United waliongeza ofa yao kwa mchezaji huyo, ofa ya kiasi cha £30m kwa ajili ya kumpata mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, ila taarifa toka Hispania zinasema kwamba ofa hiyo imekataliwa na klabu yake.

“Fabregas hauzwi,” chanzo cha Barcelona kilisema siku ya Jumatatu. “Rais (Sandro Rosell) amekuwa muwazi kwa Man United.”

Mwanzoni United walianza kwa kutoa ofa ya £25m ambayo pia alikataliwa na mabingwa hao wa Hispania, licha ya kuwepo kwa ushawishi wa Robin van Persie na David de Gea, mlinzi wa zamani wa United Gerard Pique amewaeleza Mashetani Wekundu kuachana na mbio zao za kumfukuzia mchezaji mwenzake sababu haendi popote.

“United wanapoteza muda wao,” alinukuliwa na gazeti la The Sun. “Ilimchukua muda mrefu kwa Cesc kuzirudisha ndoto zake nyumbani na hatokata tamaa.”

“Hapa ni nyumbani, ndipo ambapo familia yake ilipo, na anacheza na marafiki zake wa karibu. Ametuambia kwamba yupo na furaha na kwamba ana nia ya kuendelea kukaa na Barcelona.”

Barcelona bado haijatoa taarifa rasmi juu ya uteuzi wa Gerardo Martino kama mbadala wa Tito Vilanova kwenye kiti cha ukocha wa klabu hiyo, ila inaaminika kwamba klabu hiyo itatoa taarifa hivi karibuni.

“Hapa ni nyumbani,
ndipo ambapo familia yake ilipo,
na anacheza na marafiki
zake wa karibu.”
 
Beki wa Barca
Gerard Pique

No comments:

Post a Comment