Rihanna Aangusha Chozi Kwenye Tamasha

Rihanna
Rihanna alishangazwa na kushtushwa kwa namna alivyopokelewa na kukaribishwa na washabiki wake nchini Ufaransa, kilikuwa ni kitu kikubwa ambacho kilimfanya nyota huyo atokwe na machozi.

Akiwa kwenye tamasha lililofanyika kwenye jiji la Lille mapema wiki hii, mshindi huyo wa tuzo za Grammy aliuguswa sana mara baada ya kuimba wimbo wake wa “Stay.”

“Asanteni sana,” Rihanna alisema kwa mashabiki wake.


Na mara baada ya kukuaa kimya kwa muda akaongeza, “Siamini hiki kitu. Wote mnanifanya niwe na furaha sana.

Hiki ndio kitu pekee kinachojalisha kwangu. Na kusimama hapa na kupata upendo huu. Ziara ya Diamonds inakaribia kufika ukingoni na sikipindi hiki kitu. Sipendi kusema kwaheri. Ninyi watu mmenionyesha upendo wa juu ndani ya ukumbi kwa usiku huu. Nawapenda.”

Washabiki wake walipoendelea kupiga kelele ndani ya Grande Stade Arena, Rihanna alisema, “Sijui hata kwa nini ninalia. Ni ujinga. Nawapenda wote. Ni ziara ya Diamonds, na unajua hatuwezi ondoka kamwe.”

And leave she did not, continuing on with the show and belting out her tune “Diamonds.”

No comments:

Post a Comment