Picha za Kwanza za Mtoto wa Kate Middleton na Prince Williams Zatoka (PICHA)

Kate, William na Mtoto Wao
Dunia imeshuhudia kwa mara kwanza mtoto ambaye anategemea kuja kuwa mfalme akitoka kweye hospitali akiwa amebebwa na wazazi wake jioni ya jana Jumanne, mtoto ambaye mpaka sasa bado hajapewa jina.
 
Prince William na Kate walipungia watu mikono huku wakiwa wanafurahi huku kamera zikiwa zinawapiga picha katika muda ambao walikuwa wanatoka kwenye hospitali binafsi ya St. Mary's iliyopo Lindo Wing ndani ya jiji la London.

Duchess wa Cambridge alisema: 'Ni kitu cha kugusa hisia. Mzazi yeyote ataelewa hisia hizi zinafananaje hasa.'

Alionekana yuko poa kama mama mpya, hebu cheki baadhi ya picha hapo chini........
Kate na Mtoto Wake

William Akiwa Amembeba

Mtoto Kwenye Kitenga

No comments:

Post a Comment