Mwisho wa Usajili Sauti za Busara ni July 31, 2013 Msanii Inakuhusu Isome

Tamasha la Busara
Je wewe ni msanii wa muziki wa kiafrika? Mwisho wa maombi kwa ajili ya tamasha la 11 la Sauti za Busara ni tarehe 31/07 kwa wasanii wote wa ndani na wa kimataifa.

Tamasha litakuwa kwa siku nne kuanzia tarehe 13-16 Februari 2014. Fomu ya maombi kwenye tovuti yetu ipo HAPA au unaweza fika ofisini kwetu iliyopo Maisara mkabala na Golf Club.

Vikundi zaidi ya 250 vimeshafanya maonyesho yao katika Tamasha la Sauti za Busara, na vyote vikifanya maonyesho ya moja kwa moja (100% Live).

Zingatia tunapokea maombi mengi kila mwaka na tunaangalia na kusikiliza kila moja kwa umakini.

Tafadhali kuwa mstahamilivu kwani jopo la uchaguzi litakaa mwanzoni mwa mwezi wa nane na kuwataarifu wasanii wote waliochaguliwa na wasiochaguliwa.

Maombi yako lazima yawe :

•Umejaza fomu kwenye tovuti yetu au kwenye fomu ya karatasi, na kuambatanisha maelezo ya kikundi yasiyozidi maneno 1000.
•Nakala zako mpya 1 au 2 (CD au DVD)
•Picha 1 au 2 (JPG au za karatasi)
Tafadhali tuma nakala zako, Picha an au nyaraka nyingine zozote kwa anuani ya ofisi yetu hapo chini:


BUSARA PROMOTIONS PO BOX 3635 STONE TOWN, ZANZIBAR, TANZANIA

No comments:

Post a Comment