Mpigania Haki za Mashoga Auwawa Kikatili

Eric Lembembe
Mpigania haki za mashoga nchini Cameroon amekutwa amekufa nyumbani kwake Yaounde baada ya kuteswa, Wapigania Haki za Binadamu wamesema.
 
Mwili wa Eric Lembembe ulikutwa kwenye jiji hilo mnamo siku ya Jumatatu huku ukionekana alikuwa ameteswa vibaya sana, kundi hilo lilisema kwenye maelezo yako mnamo siku ya Jumanne.
 
“Maraiki wa Lembembe waliukuta mwili wake mnamo siku ya Jumatatu jioni. Kwa mujibu wa rafiki zake shingo yake ilivunjwa na uso wake, mikono na miguu viliunguzwa moto kwa kutumia pasi,” taarifa ilisema.
 
Shirika hilo limeelezea kitendo hicho kama ni cha “mauwaji”na kuzitaka mamlaka husika kuendelea kufanya uchunguzi wa kina.

No comments:

Post a Comment