Msichana Afariki Alipojaribu Kupokea Simu Ikiwa Kwenye Chaji

 
Majirani wa msichana mwenye umri wa miaka 23 kutoka Kaskazini Mashariki ya China kwenye mji wa Xinjiang Uygur, wametaarifu kuwa mwanamke huyo alikufa kutokana na shoti ya umeme iliyotokea wakati anapokea simu aina ya iPhone.

Dada mkubwa wa marehemu Ma Ailun alisema, mnamo siku ya Jumamosi kupitia Sina Weibo, mtandao unaotumika kama twitter nchini Chini, kwamba Ma alipigwa na shoti ya umeme wakati akijaribu kupokea simu hiyo ya iPhone wakati akiwa anaichaji.

Ma Ailun alinunua simu ya iPhone mnamo mwezi December kwenye duka linalouza vitu vya Apple na alikuwa anatumia chaja orijino kuchajia simu hiyo wakati tukio hilo linatokea, alisema dada yake.

No comments:

Post a Comment