Said Mwema |
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi alisema majambazi wapatao kumi waliokuwa na silaha nzito za kivita asubuhi ya Jumatatu waliteka mabasi mawili ya abiria yaliyokuwa yakielekea katika majiji ya Arusha na Dar es Salaam.
Alisema silaha zilizoonekana eneo la tukio ambazo zilitumiwa na majambazi kujihami ni SMG sita na LMG mbili.
Kwa mujibu wa Kalangi, mabasi yaliyotekwa ni NBS lililokuwa likielekea Arusha na RS lililokuwa likielekea Dar es Salaam,ambapo kabla waliteka gari dogo na kulitumia kufunga barabara katika hali iliyoonekana lilikuwa limeharibika.
Katika tukio hilo, abiria mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Fredrick Rugaihura (47)mkazi wa mjini Bukoba alijeruhiwa shingoni kwa risasi, ambapo majambazi hao walipora mali mbalimbali za abiria zikiwemo fedha na simu.
CHANZO: Gazeti MWANANCHI
No comments:
Post a Comment