Licha ya Kuwa ni Mke wa Mchungaji Meagan Good Ajiachia Kiutupu

Megan Good

Muigizaji maarufu wa filamu Meagan Good, ambaye anajulikana zaidi kwenye nafasi yake ya uigizaji kama Mya ndani ya filamu inayotamba ya Think Like A Man, hivi karibuni kwenye tuzo za BET alijiachia kwa kuonyesha baadhi ya sehemu zake nyeti.

Imekuwa ikielezwa kwamba Meagan ameolewa na Mchungaji Devon Franklin, ambaye inasemekana walikuwa kwenye mahusiano kwa muda wa miezi 10 kabla ya kuingia kwenye maisha mapya.


Japokuwa hakuwahi kulelewa au kuishi kwenye mazingira ya Kikanisa, ila amekuwa akisema kwamba yeye ni Mkristu na anajichukulia kama mtu wa imani na mara nyingi amekuwa akisema kwamba hatokuja kufanya mambo anayaona kama ni ya kumvunjia heshima Mungu na kwamba Yesu ni mkombozi.

Ila alipofika kwenye Tuzo za 2013 za BET kwenye ukumbi wa Nokia Theatre L.A. ndani ya Los Angeles, California mnamo siku ya Jumapili, mwigizaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alionekana kama anakinzana na kile alichokuwa akikisema kutokana na aina ya kivazi alichokuwa amekivaa.


Mcheki kwenye picha hapo chini.........



No comments:

Post a Comment