BBATheChase: Mama Yake na Selly - ‘Binti Yangu Hakufanya Ngono na Nando’

Selly na Nando Kitandani
Benedicta Galley, mama wa mshiriki toka Ghana ndani ya jumba la Big Brother aitwaye Selly, amejitokeza na kufunguka huku akikana kwamba binti yake alifanya ngono na mshiriki wa Tanzania aitwaye Nando.

Msichana huyo mrembo toka Ghana, Selly amekuwa kwenye shutuma kali mara baada ya yeye na Nando kulala usiku kucha huku wakiwa wamejifunika blanketi na Nando akiwa nyuma wa mwili wake kwa usiku wote.

Watazamaji, mimi nikiwa ni mmoja wapo: ilionekana kama wawili hao walikuwa wanafanya mchezo mbaya ila Benedicta Galley ambaye alifanya mahojiano maalum kwenye kituo cha Peace FM, amekanusha kile ambacho watazamaji wamekuwa wakikiamini huku akisema kwamba mtoto wake pekee, Selly hakufanya na wala hawezi kufanya uchafu kama huo.

No comments:

Post a Comment