Jamaa Akimbia Uwanjani Akiwa Kama Alivyozaliwa Kuburudisha (PICHA)


Mtu mmoja aitwaye, Wati Holmwood, 33, aliamua kuingia ndani ya uwanja wa ANZ akianza kucheza akiwa uchi wa mnyama huku mwilini mwake kitu pekee alichokuwa amekivaa ni pea ya viatu pekee.
Jamaa huyo mwenye mwili kiasi cha kutosha alikimbizwa na kudakwa na walinzi kataka kile kilichochukua muda wa dakika kama moja kuuzunguka uwanjani.
Holmwood alisema alitaka kukimbia umbali wa kilometa 10 akiwa kwenye hali hiyo mara baada ya kutolewa nje ya uwanja.
Ilifahamika kwamba Holmwood aliupaka mwili wake mafuta aina ya vaseline ili kuwe na ugumu wa kumshika pale atakapokamatwa na watu wa vyombo husika kwenye zoezi hilo.
Juhudi zake zilimkuta akiishia hospitali ya Auburn iliyopo ndani ya jiji la Sydney huku gazeti la Telegraph likitaarifu alionekana akiwa "amechanganyikiwa na hajielewi" baada ya kuamka na kujikuta kwenye hali aliyokuwa nayo.
Cheki pilika zilivyokuwa kwenye picha hapo chini....


No comments:

Post a Comment