Inashangaza: Kichwa cha Abiria Kwenye Ajali ya Gari Chapenya Kwenye Kioo cha Mbele Ila Amepona (PICHA)

Hii Sio Graphics
Mwanamke huyo hapo juu ambaye hakuwa amevaa mkanda wakati ajali hiyo inatokea alisukumwa na kujikuta anatokeza mbele ya kioo cha gari hii.

Abiria huyo licha ya kichwa chake kupenya kwenye kioo alifanikiwa kupona.

Gari hilo liligonga nyuma ya roli na mwanamke huyo ambaye hakuwa amevaa mkanda alisukumwa mbele.

Kichwa chake kilibanwa na kioo hicho ha gari hiyo na kujikuta anashindwa kutoka kwenye ajali iliyotokea kwenye jiji la Guizhou kusini mwa China.

Waokoaji walifanikiwa kumtoa mwanamke huyo aliyekuwa hajitambui kwa uangalifu wa hali ya juu, huku wakijaribu kutanua na kuvunja tundu la kioo hicho lililokuwa limezunguka shingo yake kitendo kilichofanikisha zoezi hilo.

Cha kushangaza, kwa mujibu wa madaktari, wote wawili dereva na abiria hawako kwenye hali ya hatari na wanaendelea vizuri huku wakipata matibabu hospitalini.

Angalia picha za uokoaji hapo chini....


Waokoaji Wakiwa Kazini


Hapa Wamefanikiwa Kumuokoa

Funzo: Vaa mkanda wa kiti cha gari kila wakati....!

No comments:

Post a Comment