Bi Harusi Ajirusha Toka Ghorofa ya Saba Baada ya Kupigwa Chini Siku ya Ndoa (PICHA)

Hatari Lakini Salama
Mwanamke mmoja wa nchini China alijaribu kutaka kujiua mara baada ya mchumba wake kumtema siku ya harusi.

Alikuwa kwenye nyumba ya baba yake akisubiri gari aina ya JEEP ambalo lilikuwa limchukue kumpeleka kwenye eneo inapofanyika harusi hiyo.

Mume wake mtarajiwa alimpigia simu kwenye simu ya mkononi na kumueleza kwamba amesitisha kufunga naye ndoa, kitendo ambacho msichana huyo aliona kuwa ni jambo la aibu na fedheha kwake.

Huku ukizingatia kwamba mwanamke huyo tayari alisha vaa shela kwa ajili ya harusi hiyo, hakika alichanganyikiwa na kutaka kujiua kwa kuruka kupitia dirishani kwenye toka gorofani ya saba.

Alikiepuka kifo kwa bahati tu mara baada ya shela lake kunasa kwenye dirisha wakati anaruka na rafiki yake kufanikiwa kulikamata shela ikiwa pamoja na msaada wa watu wengine pia.


Je unaweza kufanya kitendo kama hiki ikitokea hali kama hii au inayofanana nayo...?

No comments:

Post a Comment