Drogba na Familia Yake Wakila Raha Kwenye Boti Yake ya Kifahari


Didier Drogba anaweza kuwa ni mchezaji wa mpira wa miguu ila pia anaonekana kuwa ni mpenzi wa mchezo wa ngumi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alionekana akiwa amevaa T-shirt yenye picha ya Mike Tyson alipokuwa akila raha pande za St Tropez na familia yake.

Didier alijikoki na pensi nyeusi akiwa na na kofia nyeusi aina ya hat kimtoko kwa upande wa kivazi kukamilisha mlo wake wa mchana.

Mara baada ya kupata msosi kwenye mgahawa Didier, mke wake Diakité Lalla sambamba na watoto wao watatu Isaac, Iman na Kieran waliamua kurudi na kupumzika kwenye boti yao ya kifahari.

Familia hiyo ilifurahi kwa pamoja na kupata lunch ndani ya Le Club 55 iliyopo fukwe za Pampelonne sehemu ambayo ni mashuhuri kwa sura za watu mashuhuri.


Mcheki kwenye picha hapo chini....



No comments:

Post a Comment