Bi Harusi Afariki Saa Moja Kabla ya Kufunga Ndoa

Marehemu Levina Mmasi akilishwa chakula na aliyetarajia kumuoa, Kasisi Masawe kwenye hafla ya kuagwa kwake  (Send-Off Party) iliyofanyika Jumatano iliyopita.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Bibi Harusi ambaye ni mkazi wa Chanika mjini Handeni, Levina Mmasi (23) amefariki dunia saa moja kabla ya ndoa yake kufungwa katika Kanisa la Katoliki la Roma Wilaya Handeni Jumamosi na hivyo kuilazimu kamati ya maandalizi ya harusi kujigeuza na kuwa ya msiba.

Kifo hicho kilichotokea Jumamosi mwishoni mwa wiki iliyopita, kimekuwa gumzo mjini Handeni huku wananchi wakisema kuwa ni tukio ambalo halijawahi kutokea katika wilaya hiyo.

Msemaji wa familia ya marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Firmin Mrimasha, alisema kuwa chanzo cha kifo cha Levina ambaye alijifungua mwanzoni mwa wiki iliyopita,ilikuwa ni homa aliyoipata ghafla siku ya Alhamisi na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni na kukutwa na malaria na kisha kulazwa kwa matibu.


CHANZO: Gazeti la MWANANCHI

No comments:

Post a Comment