David Moyes Asisitiza Mshambliaji wa Man U Wayne Rooney Hauzwi

Wayne Rooney
Meneja wa Manchester United David Moyes kwa mara nyingine tena amesisitiza kwamba Wayne Rooney hauzwi, na hii ni baada ya Chelsea kusema kwamba mshambuliaji huyo wa Uingereza ni mtu wanayemtaka kwa udi na uvumba.
 
Akiongea na waandishi mjini Sydney, bosi huyo wa United alisema: "Msimamo wa klabu haujabadilika."
 
Moyes pia yupo kwenye mchakato wa kuhakikisha lengo lake la kumpata kiungo mchezaji wa Barcelona Cesc Fabregas linafanikiwa.
 
Alisema: "Nawasiliana na mtendaji wetu mkuu ambaye anafatilia mpango huo na natumai kufahamu zaidi ndani ya siku au zaidi."
 
Bosi mpya wa Chelsea mreno Jose Mourinho alishaonyesha nia yake ya kumtaka Rooney japo ofa yake ilikataliwa.

"Tunajaribu kwa nguvu sana
kuongeza wachezaji"
 
David Moyes
Bosi wa Man Utd
 
CHANZO: BBC Footbal 

No comments:

Post a Comment