Usain Bolt Ashindwa Kutamba Mbele ya Justin Gatlin Kwenye Mbio za Mita 100 Zilizofanyika Rome


Mkimbiaji wa mbio za mita 100 toka nchini Marekani Justin Gatlin amefanikiwa kumshinda bingwa mara sita wa mashindano ya Olimpiki Usain Bolt kwenye mbio za Golden Gala, Diamond League, zilizofanyika leo nchini Italia ndani ya jiji la Rome.

Justin alimshinda Usain kwa zaidi ya nukta moja ambayo ni sawa na asilimia moja.

Justin alibidi atumie maarifa ya ziada ya kukitanguliza kichwa chake mbele zaidi kwenye mstari na kuweza kushinda kwa kutumia sekunde 9.94 na Usain akifata kwa kutumia sekunde 9.95.

No comments:

Post a Comment