Mourihno Amsambulia Ronaldo: Anajiona Kama Anajua Kila Kitu
Jose Mourinho amefuta ndoto za kuambatana na Cristiano Ronaldo kuungana naye kwenye timu ya Chelsea baada ya kukiri kwamba uhusiano wao ulivunjika walipokuwa pamoja kwenye klabu ya Real Madrid.
Chelsea walikuwa wanahusishwa na uhamisho wa paundi millioni 60 kwenye kipindi cha majira ya joto ili kuweza kumchukua winga huyo sambamba na timu za Manchester United na Paris Saint-Germain ambazo nazo zinamuwinda.
Ila Mourinho, ambaye ameanza awamu ya pili kuifundisha timu hiyo ya Stamford Bridge mnamo siku ya Jumatatu, amesema kwamba wawili hao walishindwana katika kipindi cha mwisho katika miaka mitatu ambayo Meneja huyo aliitumikia timu hiyo kwa kile alichosema kwamba mchezaji huyo 'alidhani alijuua kila kitu'.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment