Kanye West Kuachana na Kim Kardashian

Kanye na Kim
Kwa mujibu wa blog ya US Celebrity, mahusiano ya watu wawili mashuhuri yanaonekana kuwa na vikwazo vya hapa na pale.

MediaTakeOut imeripoti;
 

Tumekuwa tukipokea taarifa za kushangaza kwamba Kim Kardashian na Kanye West huenda wakawa wameachana.
 
Kwa mujibu wa mtu wa ndani, amesema kwa siku za karibuni wawili hao wamekuwa wakigombana na zaidi ni juu ya vyombo vya habari ambapo Kim na Kanye wamekuwa wakifatiliwa navyo kwa kiasi kikubwa.

Wiki iliyopita kwenye shughuli ya kumpongeza Kim kwa kutarajiwa kuwa mama mambo mengine yalijitokeza.


Mtu mmoja wa karibu na Kanye alisema, "hakika Kanye anajaribu kumpa Kim kila kitu anachokihitaji. Anafahamu kwa kiasi gani (kipindi chake) nini kinamaanisha kwake, naye anampenda sana kwa kuonyesha kumuunga mkono kwa hilo. Ila sivyo ambavyo yeye alivyo."

Mtu huyo toka ndani aliendelea, "[Kanye] sio aina ya mtu ambaye anahitaji kamera kwa kila jambo analolifanya, ila ndivyo ambavyo Kim alivyo."

Tumeelezwa kwamba Kanye alimuacha Kim Los Angeles muda mchache baaada ya shuguli hiyo, na haina uhakika kama ana mpango wa kurudi.


Kuzongwa na kamera kila wakati sio ishu pekee. Kanye anakabiliana na jukumu kubwa kuwa makini na jamii juu ya ujio wa album yake mpya. Mtu huyo wa ndani pia alisema, "Kanye kwa sasa yupo Hawaii, nafikiri anafanya kazi za kimuziki. Ila pia nafiki yamekwisha kati yake na Kim."

No comments:

Post a Comment