Papa Wemba Akanusha Uvumi Juu ya Kifo Chake


Mapema hapo jana, mmoja kati ya wanamuziki mashuhuri toka Afrika Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu kama Papa Wemba alivumishiwa kuwa amefariki.
 
Kwa sasa mwanamuziki huyo maaarufu toka Congo wa miondoko ya soukous ni mtuhumiwa mkubwa wa habari ya kuzushiwa kifo.

Mitandao mbalimbali mnamo siku ya Jumatano, June 5, 2013 ilitaarifu Wemba mwenye umri wa miaka 64 amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi, kitu ambacho kilifanya mashabiki wake wengi wanaolizunguka bara la Afrika kuwa kwenye tahamaki.

 
Ila Papa Wemba alifanikiwa kutuliza wasi huo kwa kuamua kutoka na kuzungumza mara moja.

Wemba alitoa habari hizo kupitia akaunti yake ya Twitter, akisitisha wasi huo, ‘Pumzikeni nikiwahakikishia kwamba mimi ni mzima na nipo pamoja nanyi‘, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, akiongza kwamba habari hizo zilikuwa ni za‘kizushi kizushi na zaidi ya kizushi ….‘.

Papa Wemba ni mmoja kati ya wanamuziki wa kwanza kujiunga na bendi ya muziki wa Soukous, Zaiko Langa Langa lilipoanzishwa mnamo mwezi Desemba mwaka 969.


Amefanikiwa kutoa zaidi ya album 40 mpaka sasa.....

No comments:

Post a Comment