Mwili wa Mangwea Kuwasili Dar Leo Saa Saba Mchana


Mwili wa marehemu Albert Mangwea unategemea kuingia nchini leo majira ya saa saba mchana kwa mujibu wa Kamati ya Mazishi ya msiba huo.

Maandalizi mpaka sasa yanakwenda sawa huku ukiwa unasubiriwa mwili majira ya saa saba taarifa hiyo ilisema huku ikiongeza, mara baada ya kuwasili mwili utapelekwa moja kwa moja kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuhifadhiwa.

Kesho Jumatano kuanzia saa mbili asubuhi mwili wa Mangwea utapelekwa kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni ili Wananchi waweze kutoa heshima za mwisho, mchana mwili utasafirishwa kwenda Morogoro kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika siku ya Alhamisi.

Picha chini ni gari litakalotumika kubeba mwili wa Mangwer.




Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Albert Mahala Pema Peponi ......

No comments:

Post a Comment