Dully - Niliahirisha Show Kumi Ili Nimzike Mangwea (AUDIO)

Dully Sykes

Msanii mkongwe kwenye game ya Bongo Fleva Dully Sykes imembidi kuahirisha show zake alizokuwa amepanga kuzifanya Kanda ya Ziwa mwishoni mwa wiki ili aweze kushiriki kwenye mazishi ya msanii mwenzake Albert Mangwea.

Mwanzoni nilipoongea naye nilitaka kujua kwa vile alivyoupokea msiba huu Dully alisema, "Msiba kwangu mimi ni mkubwa ni mkubwa sana siwezi kuuelezea, ni kwa sababu nilikuwa na show 12 Kanda ya Ziwa na nimepiga show mbili tu mwisho."

Dully aliendelea kwa kusema, "Jumamosi nikawasha gari Jumapili nikaenda kulala Dodoma, Jumatatu nikaingia Morogoro nikisubiria mwili wa ndugu yangu ili niupumzishe na show zingine zilizobakia nimezikatisha, show kumi." Alisema Dully.

Sikiliza hapo chini Dully akiongea....


No comments:

Post a Comment