Jay Z na Beyonce Pamoja Kwenye Steji (PICHA)


Beyonce alimualika Jay Z kuungana naye kwenye jukwaa juzi kwenye tamasha lililoitwa Sound Of Change lililofanyika kwenye uwanja wa Twickenham nchini Uingereza.

Umati uliokuwapo kwenye tamasha hilo ulichanganyikiwa pale Jay Z alipotokea kwenye jukwaa sababu hakuna hata mmoja aliyekuwa akitegemea ujio wake.

Kwa pamoja waliimba wimbo wa "Crazy In Love".



Hakika ilipendeza...

No comments:

Post a Comment