Muigizaji Toka Bollywood Jiah Khan Ajinyonga Baada ya Kuumizwa Moyo
Mwigizaji mchanga wa kike toka Bollywood Jiah Khan amekutwa amefariki kwa kujitundika kwenye kitanzi nyumbani kwake Mumbai eneo la Juhu.
Taarifa toka kwa jeshi la Polisi zinasema kwamba sababu ya kifo chake kilichotokea usiku wa juzi imetokana na kuumizwa moyo juu ya mapenzi yaliyoshindikana na mmoja wa watoto wa muigizaji mmoja.
Mwili wa Jiah, 25, ulikutwa ukiwa unaning'inia nyumbani kwake maeneo ya ‘Sagar Sangeet’ ndani ya Juhu usiku wa juzi sehemu ambayo amekuwa akiishi na mama yake na dada yake ambao wakati anafanya maamuzi hayo wote walikuwa hawapo.
Uchunguzi wa mwanzo umebaini kwamba msichana huyo alikuwa na mahusiano na Suraj, ambaye ni mtoto wa waigizaji maarufu Aditya Pancholi na Zarina Wahab kwa kipindi cha karibia mwaka hivi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment