Naomi Campbell Amtimua Kazi Mwanamitindo kwa Kutoka na Mpenzi Wake wa Zamani


 
Mwanamitindo mmoja toka China, Luo Zilin, ambaye alikuwa ni mshindi wa wa pili kwenye mashindano ya mitindo yaliyoandaliwa na Naomi yaliyojulikana kama 'The Face' amefukuzwa kazi na uongozi wake.

Taarifa hiyo inasema kwamba sababu ya kufukuzwa kazi imetokana na kile kilichosemwa kuwa ni kitendo chake cha kuvunja maadili ya taaluma na vitendo visivyokubalika kazini, hii ni mara baada ya kupigwa picha akiwa na ana-kiss na aliyekuwa mpenzi wa Naomi, billionea aitwaye Valdimir Doronin.

Mwanamitindo huyo ambaye aliwahi kutwaa taji la Miss Universe nchini China alichukuliwa na Naomi Campbell na kuingizwa kwenye kipindi cha Tv cha mitindo na kuna dalili zinazoonyesha kwamba  Luo na Vlad walifahamiana kupitia Naomi.

Neal Hamil, Rais wa MIX Model Management NYC, amethibitisha kuvunjwa kwa mkataba wao na mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 25.


Luo na Naomi Campbell
Luo na Vlad
Luo Aliposhinda Miss Universe
Naomi na Vlad
Usifanye mchezo na Naomi Campbell kwa mpenzi wake wa zamani....

No comments:

Post a Comment