Cheki Hapa Picha za Mamia ya Watu Waliompokea Mangwea Toka Airport

Sehemu ya Umati Uliojitokeza
Baadhi ya barabara za jiji la Dar ilibidi zifungwe na magari kutoweza kutembea kwa muda mara baada ya msafara toka Uwanja wa Ndege kuelekea Hospitali ya Muhimbili kuanza.

Mamia ya wananchi kwalijitokeza kuupokea mwili wa Msanii wa Kizazi kipya Albert Mangwea aliyefariki nchini Afrika Kusini wiki iliyopita.

Mara baada ya mwili wa Mangwea kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Kambarage Nyerere na kuanza msafara kuelekea Hospitali ya Muhimbi kwa ajili ya kuhifadhiwa, mamia ya watu waliakusanyika kutaka gari lililobeba mwili wa Mangwea lisukumwe.

Mwanzoni gari lilianza kuondoka taratibu kufuata Barabara ya Nyerere ila watu waliojitokeza wengi wao wakiwa ni Vijana waligoma gari hilo kuendeshwa na kutaka lisukumwe mpaka Hospitali ya Muhimbili.

Chini ni baadhi ya picha za msafara huo kwenye barabara ya Nyerere eneo la Tazara...




Katikati Ni P Funk Majani Akiongoza Msafara

P Funk Majani Akiwa Amebeba Msalaba

Barabara Zilizingirwa na Watu

Wanawake kwa Wanaume


Polisi Nao Walikuwepo

Ni Mchakamchaka

Barabara ya Nyerere Ilimezwa na Watu

Watu Wakiwa Wamelizunguka Gari

Hakika Watu Walikuwa ni Wengi


Gari Lililobeba Mwili wa Ngwear

Hapa Kama Linaongozwa Hivi

Wanahabari Nao Walikuwepo

Ilibidi Gari Lisukumwe

Polisi Wakiwa Nyuma ya Msafara

Kila Mmoja Alitaka Kuligusa Gari

Na Ndivyo Ilivyokuwa

Nyimbo Mbalimbali Ziliimbwa

No comments:

Post a Comment