Mtoto wa MichaelJackson Akimbizwa Hospitali Baada ya Kujaribu Kujiua


Paris Jackson mapema leo siku ya Jumatano alikimbizwa hospitali kwa kile kinachoelezwa kuwa alitaka kujiua.

Mama yake Debbie Rowe inaaminika naye amekiri kuhusiana na taarifa hizo akisema binti huyo mwenye umri wa miaka 15 kwa sasa yupo hospitali jijini Los Angeles.

Wakili wa Katherine Jackson, ambaye ni Bibi wa Paris naye alijitokeza na kuthibitisha habari juu ya habari hiyo ya kutaka kujiua.

"Anasumbuliwa na kitendo cha kumpoteza Baba yake", Wakili huyo alilieleza gazeti la New York Daily News.

No comments:

Post a Comment