Maombi Zaidi kwa Nelson Mandela

Nelson Madiba Mandela
Wananchi wa Afrika Kusini wamekuwa wakimuombea Mandela akiwa amelazwa hospitali kwa siku ya pili mara baada ya kiongozi huyo wa zamani kulazwa kutokana na kusumbuliwa na mapafu.

Hali ya Mandela iliandikwa kwenye magazeti mengi ya nchini Afrika Kusini ila Maafisa wa Serikali wa nchi hiyo hawajatoa taarifa yoyote mpaka sasa toka walipotoa taarifa ya kulazwa kwake mapema siku ya Jumamosi kwenye hospitali moja jijini Pretoria, taarifa iliyosema Mandela yupo "anaumwa ila anajiweza."

No comments:

Post a Comment