Joto Hasira By Lady Jay Dee (MASHAIRI)

Lady Jay Dee a.k.a Anaconda
KIITIKIO:

Hili joto hasira, ambaa
Upepo hakuna Ambaa,
Naruka mwenyewe Yelela, yelela, ambaa.
Foleni njia nzima, ambaa
Na pesa hakuna Ambaa,
Naruka mwenyewe Yelela, yelela, ambaa

UBETI 1:

Kila siku nimenuna
Kwanini tunagombana
Tena tunakosoana, kama tumechanganyikiwa
Na sioni hata maana Ya si kuzinguana
Yaani kila mtu anajua sana
Au yote sababu ya?, sababu ya?

RUDIA KIITIKIO:

UBETI  2:

Mazao twalima wote
Sahani wavuta kwako
Kama chakula tule wote
Kwanini chote kije kwako
Kisu mpini umeshika wewe
Vitisho kunikata mimi mmmmhh
Au yote sababu ya? Sababu ya?

KIITIKIO:

Hili joto hasira, ambaa
Upepo hakuna Ambaa,
Naruka mwenyewe Yelela, yelela, ambaa.
Foleni njia nzima, ambaa
Na pesa hakuna Ambaa,
Naruka mwenyewe Yelela, yelela, ambaa

KIBWAGIZO:

Uuuuh, sahau sahau shida
Oooh ishi ka ziliisha jana
Say goodbye joto,
Rest in Peace Shida
Knock, knock money

GANI: Prof. Jay

Wenyewe wanasema usawa unakaba
Na rafiki wa kweli ni mama na baba
Hawa wengine wala usiwaamini
Maana binadamu wa sasa wana roho saba
Watakuwa na wewe kwenye raha
a hawatakuwa na wewe kwenye njaa
ora nipige misele yangu peke yangu
Niruke kivyangu na woga niliukataa Aaah!!
Nabadilika kama saa
Na Siku hazigandi na sitokataa tamaa
Wamejaa, usaliti na chuki
Watu wa karibu wanageuka mamluki
Jenero nasonga iwe joto au baridi naamini tutashinda
Kama mbwai iwe mbwai barida
We make more money rest in peace shida
Ukinuna unataka tunune wote
Ukilia unataka tulie wote
Vita vyako tunapigana wote
Tukishinda tushinde au bora tufe wote
Kama kulima kote tumelima wote
Hata kupanda kote tumepanda wote
Kupalilia tumepalilia wote
Aaaargggh !!! Nashangaa sasa mbona hatuvuni wote??

RUDIA KIITIKIO:

MWISHO

No comments:

Post a Comment