Khadijah Kopa Afiwa na Mumewe (HABARI MOTO)

Marehemu Jaffari Ally
Taarifa nilizozipata mapema leo alfajiri zinasema kwamba Mume wa Malkia wa Mipasho,  Bi. Khadija Kopa, aitwaye Jaffari Ally amefariki dunia usiku wa kuamkia leo mida ya saa 9 usiku, Katibu wa Bendi ya TOT Gasper Tumaini amethibitisha juu ya msiba huo.

Taarifa za awali zinasema kwamba chanzo cha kifo chake ni ugonjwa wa Maralia, ambapo siku ya Jumatatu marehemu Ally alipelekwa Hospitali ya Lugaro kwa ajili ya kupata matibabu.

Taarifa zaidi zinasema kwamba marehemu alipata nafuu na kurudi nyumbani kwao Bagamoyo, hali ambayo ilimpelekea Khadija Kopa kusafiri kikazi, na inasemekana mpaka umauti unamkuta Jaffari Mkewe Khadija Kopa alikuwa yupo kikazi mikoani kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki.

Pole sana Bi. Khadija Kopa kwa kumpoteza Mumeo Mpendwa, Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu. 

Hapo chini nimeweka baadhi kumbukumbu za picha kwenye matukio mbalimbali ambayo marehemu Jaffari alikuwa na mke wake Khadija Kopa...


 


 

 
Mungu ailaze roho ya Jaffari Ally mahali pema peponi.... Amin.

Taarifa zaidi juu ya Msiba huu nitaendelea kukuletea kwa kadiri nitakavyokuwa nazipata....

No comments:

Post a Comment