Utata wa Uraia wa Msichana Anayesemekana ni Mtanzania Ambaye Anayetarajiwa Kunyongwa Ijumaa Hii Nchini Misri Wajitokeza

Fatma a.k.a Brown Berry
Utata juu ya uraia wa Msichana aliyekamatwa na madawa ya kulevya na kisha kuhukumiwa kunyongwa Ijumaa hii nchini Misri umejitokeza.
 
Wapo ambao wanasema msichana huyo ni Mtanzania ambaye anafahamika kwa jina la Fatma a.k.a Brown Berry ambaye inasemekana anaishi Ilala jijini Dar es Salaam na kuna ambao wanasema wanamfahamu huyu binti kuwa ni raia wa Oman aliyezaliwa Tanzania.

Chanzo cha kwanza kupitia Jamii Forum kiliandika, "Kwanza naanza kukukosoa mleta uzi, huyu binti sio Mtanzania, ni raia wa Oman aliyezliwa Tanzania, pia huyo sio mwanae hana mtoto huyu binti, na pia haishi Ilala anaishi Muscat, hayo mengine sema mwenyewe, Wewe umehadithiwa habari zake mimi namfahamu vizuri."
 
Kisha chanzo cha pili katika kuunga mkono chanzo cha kwanza kiliandika, "Naweza kukubalia na wewe. Ukiangalia passport yake imeandikwa kiaarabu ambapo kwa Tanzania hawatumii hiyo Lugha. Hata arrangement tu ya passport inaokujulisha kuwa si ya Tanzania. Pengine watu walisikia anaongea Kiswahili au alisema anatokea Tanzania wakajua ni Mtanzania. Swali la kujiuliza alikuwa anatoka wapi na anaelekea wapi?
 
Chanzo cha tatu kwa kupinga alichosema chanzo cha kwanza na cha pili nacho kikaandika, "Huyu ni Mtanzania alieishi muscat lakini anajulikana hadi alipokuwa akiishi wala tusibishe, ni sawa na watanzania waliokwenda uk kutafuta maisha takriban wote wana paspot za uk lkn watanzania, huyu dada ni Mtanzania na anajulikana msibishe." 

Fatma a.k.a Brown Berry
Je upi ni ukweli juu ya uraia wa msichan huyu....?

No comments:

Post a Comment