BBA The Chase: Muwakilishi wa Zimbabwe Pokello Kwenye Wakati Mgumu Sababu ya Mkanda Wake wa Ngono

Pokelo Nare
Kurasa kibao kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook zimeanzishwa huku zikimshambulia muwakilishi toka Zimbabwe kwenye jumba la Big Brother Pokello Nare sababu ya mkanda wa ngono aliowahi kuutengeneza miaka ya nyuma na mpenzi wake aitwaye Desmond ‘Stunner’ Chideme.

Ukurasa uliopewa jina la ‘Bring Pórnello Home’, ulianzishwa wiki iliyopita na mpaka sasa una wanachama zaidi ya 6000 unaoufatilia.

Mpango wa Kiongozi wa ukurasa huo ni wa kutaka kuungwa mkono na mashabiki wapige kura ili Pokello atoke nje ya mchezo.

Kwa mujibu wa kiongozi wa ukurasa huo ameandika, Pokello ni nyota wa ngono ambaye wao wanaona kwamba asingeruhusiwa kuiwakilisha nchi sababu ya tabia yake mbaya”.

“Pokello ni nyota wa ngono anayejulikana sana, kwa hiyo ni kitu gani anachokifanya kwenye show ya Big Brother Afrika show? Sio kwamba sisi ni tunamchukia, ila tupige kura arudi nyumbani,” aliandika kiongozi wa kundi hilo.

No comments:

Post a Comment