Sitaki Kusikia Nyimbo za NGWEAR Alizorekodi Bongo Records Zikipigwa Clouds fm (UJUMBE)

P Funk a.k.a Majani
Producer mkongwe wa Muziki wa Kizazi Kipya P Funk Majani amefunguka na kusema hataki kusikia Stesheni ya Clouds fm ikipiga wimbo wowote Marehemu Mangwear uliotengenezwa kwenye studio yake ya Bongo Records ukichezwa kwenye kituo hicho.
 
Kwenye SmS aliyoituma na binafsi kuipata Producer huyo ameanza kwa kutoa rambirambi zake na kumuelezea Ngwear kwake yeye kama moja kati ya nyota ing'aayo
 
Akiendelea na kuonyesha kuushtumu Uongozi wa kituo hicho kwa kuhusika kwa namna moja ama nyingine kwa kumsababishia msongo wa kimawazo uliompelekea kuanza kutumia madawa ya kulevya kitu ambacho inaaminika ndicho kilichosababisha kifo chake.
 
Soma ujumbe wa Maandishi alioutuma P Funk Majani hapo chini.....
 

No comments:

Post a Comment