P Funk Majani |
Leo nilipata fursa ya kuongea na mmoja kati ya maproducer wakongwe kwenye tasnia ya Muziki wa hapa Bongo aitwaye P Funk Majani.
Mahojiano yalikuja mara baada ya taarifa zilizosambazwa mapema leo kwamba Producer huyo amekataza nyimbo zilizorekodiwa na Mwanamuziki aliyefariki nchini Afrika Kusini jana Albert Mangwea kuwa zisipigwe kwenye kituo cha Clouds Fm.
Mbali na mambo mengine nilitaka kujua ukweli na undani juu ya taarifa hiyo na haya ndio yalikuwa maongezi yangu na P Funk Majani...
DC: Je ni kweli kwamba umekataza Nyimbo za Ngwear zilizorekodiwa Bongo Record kuwa zisipigwe Clouds Fm..?
P Funk Majani: Hiyo ni kweli kabisa, mimi nimekereka na hili jambo kwanza kwa sababu mimi na Mangwea tumejuana miaka kibao na tumeongea mengi, so mimi nnachojua uamuzi niliochukua ni kitu ambacho yeye mwenyewe angependa na angetaka iwe hivyo....
Kwa sababu kila siku alipokuwa anakuja studio malalamiko yake ilikuwa ni kuhusu hawa hawa watu kila siku....
Umenielewa..? so ni hicho kilichokuwa kinatajika kufanyika, na mi mwenyewe sifurahi wao wafaidike, sasa hivi ambaye amefariki mtu wetu ambaye tunampenda nyie mnachukulia biashara wanatangaza, wanafanya nini, wanapiga na nyimbo, alipokuwa hai mbona mlikuwa hamumsaidii....
Mlipokuwa mnajua labda ana matatizo ya kutumia madawa ya kulevya mbona hamjamsaidia kumsaidia kumchangia kama Ray C sijui nani kumpeleka nje au wapi asafishwe basi......
So…! Vitu kama mimi basically nimechoka utawala wao sababua wao mchezo wao ni kuchezea wasanii vichwa kuwapa stress na kuwaangamiza kimaisha.....
Umenielewa… kwa udulumati wao, udhulumati wao umezidi so ndio hicho kinachosababisha watu wahanganyikie kimaisha, umenielewa…?
Kukosa fedha na kuweza kutimiza mahitaji ya maisha lazima uchanganyikiwe, unakimbilia vitu vitu suala za pombe au sijui madawa ya kulevya au nini inategemea na mtu moyo wako una nguvu kiasi gani cha kudhibiti hivi vitu.
DC: Unataka kusema kwamba jamaa ndio wamesababisha kifo chake…?
P Funk Majani: Siwezi kusema asilimia 100 wamesababisha lakini mchango mkubwa wa frustration, frustration, unajua kitu frustration…? Siwezi ku-accuse, si-accuse lakini hiyo ni maoni yangu mimi, kutokana na yale maongezi niliyokuwa nae nikikaa na mdogo wangu Mangwea, umenielewa….?
Najua kabisa alichokuwa ananiambia na vitu ndio vimemsababisha aingie huko, sasa mimi ndio sitaki kwa ufupi, kama nimekosea mtanisamehe bwana….
DC: Je umewataarifu rasmi..?
Nimeanza kwa kupiga simu kwa sababu ni asubuhi nimeamka vile nimewafahamisha, nimewaambia vizuri, nilivyowaletea hizi nyimbo niliwaletea bila mkataba au karatasi yoyote mmezipiga....
So... kwa sasa hivi kwa ustaarabu naomba nnavyowaomba acheni msizipige, na mi ntaleta official barua, nimeshaongea na Cosota, eeh watai-stamp Wakili ndio ataiandika barua inapelekwa vizuri na vitu vinaendelea, kama wao ni wastaarabu itabidi waelewe.
Sikiliza Audio ya mahojiano haya hapa chini...
No comments:
Post a Comment