Albert Mangwear a.k.a Ngwear |
Chanzo cha kifo chake inaelezwa kuwa ni kutumia madawa ya kulevya kupitiliza.
Kwa kipindi sasa Msanii huyo alikuwa nchini Afrika ya Kusini, huku ikielezwa alikwenda huko kwa ajili ya kufanya show, mara baada ya kumaliza ziara yake aliamua kujikita kwa muda katika kile kinachosemekana kufanya michongo ya hapa na pale.
Taarifa zilizotumwa na mtu wa karibu aliyejiita Hussein Original ambaye yupo jijini Pretoria amesema kwamba Magwear amefariki leo asubuhi, Hussein amesema waliamka asubuhi na kuamua kwenda kuwaamsha wenzao na ndipo walipomkuta Ngwear akiwa amefariki huku M To The P akiwa hajitambui.
Hussein alisema "Mangwear alikutwa chumbani (Ghetto) akiwa tayari amefariki huku msanii mwenzake aitwaye M To The P alikutwa akiwa mahututi na hajitambui".
Aliongeza kwa kusema "mpaka sasa M To The P bado yupo hospitali na daktari amethibitisha juu kifo cha Ngwear".
Taarifa zaidi zimeeleza kwamba wasanii hao walikuwa wanategemea kurudi nyumbani Tanzania leo hii.
Ngwear Akiwa na M 2 The P |
Wimbo wa mwisho kwa msanii huyo kutoka rasmi redioni ni Ustake Beef (Yupo Juu) ambao alimshirikisha TID, mbali na huo Ngwear alifahamika na kutamba na nyimbo kama Ghetto Langu, Mikasi, She Gotta Gwan na nyinginezo nyingi za kwake na ambazo alizoshirikiana na wasanii wenzake.
Taarifa zaidi nitajitahidi kukufikishia kadiri ntakavyokuwa nazipata....
Mungu Ailaze Roho ya Marehemu NGWEAR Mahali Pema Peponi....!
No comments:
Post a Comment