Mwili Wa Marehemu Ngwear Kufika Nchini Siku ya Jumapili
Kamati ya mipango ya mazishi ya marehemu Ngwear imetoa taarifa mpya kwamba mwili wa Albert Mangwea utafika hapa nchini siku ya Jumapili tarehe 2 June saa nane mchana na sio Jumamosi kama ilivyotaarifiwa mwanzo.
Kamati hiyo pia imeeleza kwamba sababu za mwili wa Albert Mangwea kushindwa kufika Jumamosi ni kutokana na Watanzania waishio nchini Afrika Kusini nao kuomba kutoa heshima za mwisho kwa ndugu yao.
Kutokana na hivyo taratibu zote za kuaga mwili wa marehemu Albert Mangwea kwa wakazi wa Dar zitafanyika siku ya Jumatatu tarehe 3 June kuanzia saa mbili ya asubuhi mpaka saa sita mchana kisha safari ya kuelekea Mororgoro itaanza.
Kamati inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment