Je Kutembea na Wavulana 15 ni Idadi Kubwa kwa Msichana Mwenye Miaka 22...?

 
Mara zote nilikuwa nikipanga kwamba nitabaki na bikira yangu mpaka nitakapokuja kuolewa...

Nilijitahidi kubaki na msimamo huo mpaka nilipofikisha umri wa miaka 22 bikira yangu nikaipoteza japo nilikuwa naipenda sana.

 Ni mwaka wa 4 sasa na nimeshatembea na wanaume zaidi ya 15, kwa sasa nipo kwenye mahusiano ambayo naamini yanaweza kunifikisha mpaka kwenye ndoa.

Siku moja mpenzi wangu aliniuliza kabla ya kuwa na yeye nilishakuwa na wanaume wangapi nilijisikia aibu sana kutaja idadi ya ukweli na nikamjibu watano...!

Je kutembea na wavulana 15 ni idadi kubwa..? Je ni idadi gani ya wanaume kwa umri nilionao ni sahihi...?

No comments:

Post a Comment