Clouds Media Group Yajitolea Kuusafirisha Mwili wa Mangwea

Ruge
Kampuni ya Clouds Media Group inayomiliki vituo vya Clouds FM na Clouds TV imejitolea kuusafirisha mwili wa marehemu Albert Mangwea kutoa Afrika Kusini kuja Tanzania kwa ajili ya kuzikwa.

Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds FM, Ruge Mutahaba, amethibitisha wao kuchukua jukumu hilo.

Ruge Mutahaba alisema "Tumeamua kwa mikono miwili kushiriki katika msiba huu wa ndugu yetu Mangwea.”

Taarifa juu ya Kampuni hiyo kusaidia zilianza kuenea tangu juzi mara baada ya Kamati ya Mazishi kushindwa kuweka wazi juu ya Makampuni, Taasisi au watu watakaofanikisha kuuleta mwili wa Marehemu Ngwea.

Mwili wa Mangwea amepangwa kuletwa nchini kesho Jumapili na kuagwa rasmi siku ya Jumatatu kisha kusafirishwa kwenda mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi.

No comments:

Post a Comment