Memba Wa Kundi La Kris Kross, Chris Kelly, Afariki Akiwa Na Miaka 34

Chris Kelly a.k.a Mac Daddy
Habari za kituo cha Fox zilisema, msanii hiyo alikutwa hajitambui nyumbani kwake.

Mpelelezi Betty Honey wa kliniki ya uchunguzi ya kituo cha Fulton County alisema, Kelly 34, kifo cha msanii huyo kilitokea majira ya 11 jioni kwenye kituo cha matibabu kilichopo Atlanta.
 

Bibi Honey alisema, hawana uhakika wa sababu iliyopelekea kifo cha msanii huyo, na mpaka sasa uhunguzi wa mwili wake bado haujafanywa.
 

Ila koplo Kay Lester wa kituo cha polisi cha Fulton County alisema "inaonekana kwamba kifo chake kimetokana na kula dawa kwa kupitiliza."
 

Kelly, ambaye alijulikana kwa jina la "Mac Daddy" alikuwa anaunda kund la Kriss Kross na mwenzake aitwae Chris Smith, aliyejulikna kama "Daddy Mac," mwanzoni na kati ya miaka ya 90.
 

Marapa hao walivumbuliwa na producer Jermaine Dupri, alipowakuta wanaimba kwenye kumbi moja ndani ya Atlanta.
Mac Daddy Na Daddy Mac Enzi Hizo

No comments:

Post a Comment