Balotelli Apigwa Chini Na Demu Wake Baada Ya Kusema Ataruhusu Wachezaji Wote Wa Madrid Wamlale

Mario Balotelli amepigwa chini na aliyekuwa demu wake aitwaye Fanny Neguesha siku chache mara baada ya kusema timu nzima ya Real Madrid itaweza kulala na demu wake huyo.

Gazeti la SunUk limetoa taarifa hiyo.

Mrembo huyo Fanny, 22, aliondoka kwenye nyumba ya kifahali ya jamaa huyo mtukutu na kwenda kujiachia na mbele ya safari.

Pals alisema mshambuliaji huyo wa Milan amekasirishwa na kitendo hicho cha Fanny kuondoka, kwa hasira zake Balotelli akaamua kujipoza kwa kujinunulia gari lenye thamani ya paundi 200,000 aina ya Ferrari F450.

Balotelli, 22, aliwahi kusema, wachezaji wa Madrid akiwemo na Cristiano Ronaldo wataweza kufanya ngono na Fanny kama wataweza kushinda na kusonga mbele kwenye mechi yao dhidi ya Doutmund.

Mchezaji huyo wa zamani wa Man City alisema: “Kama Real Madrid watafanikiwa na kuingia kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, nitaruhusu demu wangu alale na wachezaji wote wa Real.”

No comments:

Post a Comment