Licha ya Kuwa na Mchumba Ludacris Azaa na Mwanamke Mwengine

Licha ya kuwa tayari ameshamchumbia demu wake wa siku nyingi aitwaye Eudoxie, hali hiyo hakumfanya Ludacris kushindwa kumpa mimba msichana mwengine.

Imeelezwa hivi karibuni kwamba mwanamke mwenye ujauzito wa Ludacris ni rafiki yake wa zamani, hii ni kwa mujibu wa taarifa. Luda na Tameka Fuller kwenye picha hapo juu waliwahi kusoma darasa moja kwenye Benjamin Banneker High School iliyopo Atlanta.

Waliwahi kuwa wanatoka miaka ya nyuma na wakawa wanaendelea kuwasiliana kwa kipindi kirefu. Ludacris na Tameka wamepata mtoto wa kike, Cai Bella Bridges, mnamo December 9 huku bado akiendelea kuwa na Eudoxie.

No comments:

Post a Comment