Wafanyakazi kwenye mochwari moja nchini Kenya walipigwa na butwaa mara baada ya kusikia kelele za kuomba msaada zikipigwa toka kwenye chumba hicho na mtu aliyetangazwa kuwa amekufa.
Shuka chini kuangalia video ya tukio hilo...
Tukio hilo la ajabu na kusikitisha lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita lilikuja mara baada ya jamaa huyo aliyefahamika kwa jina la Paul Mutora kufikishwa hospitali hapo akiwa hajitambui. Wahudumu wa hospitali hiyo walijua jamaa huyo kuwa tayari alikuwa ameshafariki hivyo waliamua kumpeleka mochwari kuhifadhi mwili wake.
Imeelezwa kwamba Paul alikuwa na marumbano na baba yake ambayo yalisababisha kuamua kuchukua uamuzi wa kunywa dawa ya kuulia wadudu katika hali ya kutimiza lengo lake.
Alifikishwa hospitali akiwa hajitambui na sumu aliyokunywa ilimfanya aonekana kuwa kama amekufa.
Mpaka sasa uchunguzi unaendelea kwenye hospitali hiyo kujua ilikuwaje uzembe huo umetokea.
Angalia video hapo chini...
No comments:
Post a Comment