Ronaldo Asema Atampa Messi Tuzo ya Ballon d’Or


Nguli wa mpira wa miguu toka Brazil, Ronaldo De Lima, amesema kwake yeye tuzo ya FIFA Ballon d’Or angempa Messi mbele ya Cristiano Ronaldo, gazeti la Evening Standard limetaarifu.

Akionyesha kutokuwa na upendeleo kwa mtu anayeshea naye jina, Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 sasa, ambaye aliwahi kutwaa taji la Kombe la Dunia mara mbili yaani 1997 na 2003 alisema,  “Nitamchagua Messi kwa kuzingatia sababu za kiufundi..... Nitajaribu kuangalia mambo ya kuzingatia kuweza kuchagua nani mshindi atakuwa, ila mmi nadhani huu umekuwa ni mwaka mzuri kwake.”

No comments:

Post a Comment