KUTOKA MAGAZETINI: Diamond na Wema Watangaza Ndoa

Huku mchumba’ke, Penniel Mungilwa ‘Penny’ akifungasha virago kurejea kwao, mzee mzima Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametangaza kumuoa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.

Awali kabla ya kufikia eneo la kutangaza kuoana, Diamond aliweka wazi jukwaani kwamba yeye na Wema wamerudiana.

Baada ya shoo hiyo iliyomalizika saa moja usiku, paparazi wetu alimfuata Diamond akiwa amesimama na Wema na kuwauliza kama kweli wana nia ya kufunga ndoa. “Hilo mwana mbona lipo wazi, nataka kumuoa staa na nataka kuzaa na staa,” alisema Diamond huku Wema akiwa hapingi.


Chanzo: Global Publishers

No comments:

Post a Comment